Saturday, March 26, 2011

Kufurahisha mwanamke Katika Ngono

Jinsi ya Kufurahisha mwanamke Katika Ngono

WATU wengi (hasa baadhi ya wanaume) ama hawajui au hawajali ni kitu gani wenza/mwenza wake anataka kufanyiwa au akifanyiwa kitamsisimua (Turn on) hata kama amechoka sana.

Uchunguzi unaonyesha kuwa Wanaume wengi hasa kutoka nchi za Kiafrika hujali zaidi kumaliza hamu zao za mwili na kamwe hawajali kama wenza/Mwenza wake yuko tayari au la!.


Mf: Inasemekama baadhi ya Wanaume wa Kiafrika ambao ni wakubwa kiumri (wa zamani), au wale ambao wanathamini sana jadi zao asilia ndani ya Afrika, kitu cha kwanza watakacho kuambia mkiwa chumbani ni “njoo hapa" au "vua nguo basi” na kisha utavamiwa kabla hata wewe mwenyewe hujawa tayari na unalazwa chini kama sio unawekewa uume mbele ya uso wako.......halafu watu mnashangaa kuambiwa "mume wangu alinibaka".


Mfano huo unaonyesha ni kwa jinsi gani baadhi ya wanaume wanavyojipendelea(wabinafsi), na mara zote huweka akilini mwao kuwa wanawake/mwanamke ni chombo cha kumridhisha / kumstarehesha/ kumfurahisha na kumliwaza yeye “mwanaume”.

Napenda kusema kuwa mwanamke kama mwanadamu pia anahaki ya kuridhishwa, kustareheshwa, kufurahishwa na kuliwazwa pia.

Dhana hiyo potofu imepelekea baadhi ya makabila kuendeleza mila za kuwakusanya wasichana ktk umri wa kuvunja ungo (mwali) na kuwafundisha jinsi ya kuwaridhisha mwanaume kimapenzi “ hao wana bahati”.

Lakini kwa wale ambao hawafuati/hawana/hawazijui mila hizo wamekuwa wakifuatilia kwa makini na kuamini kila kinachoonyeshwa kwenye “Video” ailimradi tu kiwe kinahusu jinsi ya kumridhisha mwanaume kimapenzi.


Inasikitisha sana kuona pia baadhi hufuatilia hatua kwa hatua kila kinachoandikwa kwenye Magazeti na baadhi yao huamua kutafuta “Kungwi” na kulipishwa ili wapatiwe ujuzi wa kufanya mapenzi ili kuwaridhisha wapenzi wao.


Ninavyofahamu mimi ni kuwa , ujuzi, utundu katika kufanya mapenzi haufundishwi hata kidogo ila ni

-ubunifu wako,
-kujaribu,
-kuujua mwili wako na wa mpenzi wako,
-ufurahiaji wa mwili wako,
-kujiamini kwako,
-uwazi na ushirikiano wa mpenzi wako.


Ni vema jadi ikabadilishwa na swala zima la kufundishwa/fundwa liwe kwa jinsia zote mbili. Wake kwa waume wafundishe jinsi ya kuridhishana, jinsi ya kufurahia na yale mambo muhimu ya mahusiano ya kimapenzi iwe ni ndoa au mahusiano ya kudumu nje ya ndoa.

Pia ni vizuri utambue kuwa unapoamua kufanya tendo la Ndoa au Ngono ni vyema ukajua mahitaji ya mwenzio iwe mwanaume/mwanamke, jaribu kufamnyia Mwenza wako kitu/vitu tofauti na alivyokuwa akitarajia/alivyozoea ni vizuri zaidi na kutamfanya aendelee kuwa na hamu ya kuwa na wewe kwa muda mrefu “usipigwe kibuti” kwa vile unamjulia.....yaani unajua vipele vilipo na unavikuna vilivyo.

Thursday, March 24, 2011

Kulipuka Kwa Chris Brown

Chris Brown, ameomba msamaha  leo kwaajili ya tukio aliofanya jana katika kipindi cha “Good morning America”.  Ambacho alikasirika akachana shati lake na kuvunja dilisha baada ya majadiliano kuusu ex wake Rihana. Lakini swali kubwa leo hii, je kuna mtu ambaye anakubaliana na msamaha wake?

Serikali Yawapinga Marufuku Waganga

By Anthony Mayunga, Muso


WAGANGA wa tiba za jadi nchini ,wanatakiwa kuacha mara moja kudanganya watu kuwa wanatibu magonjwa kama kifua kikuu, kisukari na Ukimwi kwa kuwa sheria haziwataki kujitangazana badala yake wanapaswa kutangazwa na wanaopata tiba na kupona.

Onyo hilo kali limekuja wakati maelefu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa wanaendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge kupata tiba kutoka kwa Mmchungaji mstaafu
Ambilikile Mwasapile.

Mchungaji huyo amekuwa akitibu  magonjwa sugu yakiwemo kifua kikuu, kisukari, Ukimwi, degedege na shinikizo la damu.Onyo dhidi ya waganga, lilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Lucy Nkya, katika hotuba yake kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kifua kikuu Duniani.

yaliyofanyika  kitaifa mkoani Mara.
Alisema kuenea ugonjwa wa kifua kikuu unaenea kwa kasi kwa sababu  wananchi wanakubali kudanganywa na waganga hao.

“Nasema kuanzia sasa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji, kuwadanganya wagonjwa kuwa wanatibu magonjwa kama hayo, maana mnadanganya watu na wanazidi kufa. Hatutaruhusu tena mchezo huo, narudia ni marufuku, tiba halisi inatolewa hospitalini si kwingineko," alisema Naibu Waziri.

Alisema waganga wazuri hawajitangazi na kwamba wanaopaswa kujitangaza ni wafanyabiashara tu  ambao kazi yao kudanganya watu kwa kutumia matangazo mazuri mazuri.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo hakugusia tiba inayotolewa na Mchungaji Mwasapile, ambayo watu mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, wamewahi kuitumkia.

Akizungumzia mikakati ya serikali kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu, alisema wizara imeanza kusambaza aina mpya ya darubini za kisasa za LED, zenye uwezo mkubwa zaidi wa  kugundua vimelea vya kifua kikuu katika makohozi.

“Hadi kufikioa mwisho wa mwaka huu, asilimia 95 ya hospitali zote za wilaya, zitapata darubini hizi mpya na ifikapo mwishoni mwa 2012 hospitali zote zikiwemo za mashirika ya dini zitakuwa zimepata, vifaa vipya vya
kuoteshea vimelea vya kifua kikuu,”alisema na kuongeza.

Alisema  vifaa hivyo vitafungwa katika maabara za Hospitali za Muhimbili, Mbeya, Bugando na Kibong’oto.

Alikiri kuwa wizara hiyo inakabiliwa na upungufu wa wataalam wakiwemo mafundi sanifu wa maabara na uelewa mdogo wa jamii  kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu