Thursday, March 24, 2011

Serikali Yawapinga Marufuku Waganga

By Anthony Mayunga, Muso


WAGANGA wa tiba za jadi nchini ,wanatakiwa kuacha mara moja kudanganya watu kuwa wanatibu magonjwa kama kifua kikuu, kisukari na Ukimwi kwa kuwa sheria haziwataki kujitangazana badala yake wanapaswa kutangazwa na wanaopata tiba na kupona.

Onyo hilo kali limekuja wakati maelefu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa wanaendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge kupata tiba kutoka kwa Mmchungaji mstaafu
Ambilikile Mwasapile.

Mchungaji huyo amekuwa akitibu  magonjwa sugu yakiwemo kifua kikuu, kisukari, Ukimwi, degedege na shinikizo la damu.Onyo dhidi ya waganga, lilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Lucy Nkya, katika hotuba yake kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kifua kikuu Duniani.

yaliyofanyika  kitaifa mkoani Mara.
Alisema kuenea ugonjwa wa kifua kikuu unaenea kwa kasi kwa sababu  wananchi wanakubali kudanganywa na waganga hao.

“Nasema kuanzia sasa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji, kuwadanganya wagonjwa kuwa wanatibu magonjwa kama hayo, maana mnadanganya watu na wanazidi kufa. Hatutaruhusu tena mchezo huo, narudia ni marufuku, tiba halisi inatolewa hospitalini si kwingineko," alisema Naibu Waziri.

Alisema waganga wazuri hawajitangazi na kwamba wanaopaswa kujitangaza ni wafanyabiashara tu  ambao kazi yao kudanganya watu kwa kutumia matangazo mazuri mazuri.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo hakugusia tiba inayotolewa na Mchungaji Mwasapile, ambayo watu mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, wamewahi kuitumkia.

Akizungumzia mikakati ya serikali kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu, alisema wizara imeanza kusambaza aina mpya ya darubini za kisasa za LED, zenye uwezo mkubwa zaidi wa  kugundua vimelea vya kifua kikuu katika makohozi.

“Hadi kufikioa mwisho wa mwaka huu, asilimia 95 ya hospitali zote za wilaya, zitapata darubini hizi mpya na ifikapo mwishoni mwa 2012 hospitali zote zikiwemo za mashirika ya dini zitakuwa zimepata, vifaa vipya vya
kuoteshea vimelea vya kifua kikuu,”alisema na kuongeza.

Alisema  vifaa hivyo vitafungwa katika maabara za Hospitali za Muhimbili, Mbeya, Bugando na Kibong’oto.

Alikiri kuwa wizara hiyo inakabiliwa na upungufu wa wataalam wakiwemo mafundi sanifu wa maabara na uelewa mdogo wa jamii  kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu

No comments:

Post a Comment